Mistari ya Biblia Kuhusu Moto Ulao

Mistari 9 ya Biblia kuhusu Moto Ulao ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Waebrania 12:29

kwa kuwa “Mungu wetu ni moto ulao.”

02 Kumbukumbu 4:24

Kwa kuwa Bwana Mungu wenu ni moto ulao, Mungu mwenye wivu.

03 Kutoka 24:17

Kwa Waisraeli utukufu wa Bwana ulionekana kama moto uteketezao juu ya mlima.

04 Malaki 3:2

Lakini ni nani atakayeweza kustahimili hiyo siku ya kuja kwake? Ni nani awezaye kusimama atakapotokea? Kwa kuwa atakuwa kama moto wa mfua fedha au kama sabuni ya afuaye nguo.

05 Isaya 33:14

Wenye dhambi katika Sayuni wametiwa hofu, kutetemeka kumewakumba wasiomcha Mungu: “Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto ulao? Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto unaowaka milele?”

06 Kumbukumbu 9:3

Kuweni na hakika leo kwamba Bwana Mungu wenu ndiye atakayetangulia kuvuka mbele yenu kama moto uteketezao. Atawaangamiza; atawatiisha mbele yenu. Nanyi mtawafukuza na kuwaangamiza mara moja, kama Bwana alivyowaahidi.

07 Waebrania 10:31

Ni jambo la kutisha kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai.

na kuwapa ninyi mnaoteseka raha pamoja na sisi, wakati Bwana Yesu atakapodhihirishwa kutoka mbinguni katika mwali wa moto pamoja na malaika wake wenye nguvu. Atawaadhibu wale wasiomjua Mungu na ambao hawakuitii Injili ya Bwana wetu Yesu.

09 Nahumu 1:6

Ni nani awezaye kuzuia hasira yake yenye uchungu? Nani awezaye kuvumilia hasira yake kali? Ghadhabu yake imemiminwa kama moto, na miamba inapasuka mbele zake.

Mada zinazohusiana