Mistari ya Biblia Kuhusu Kujisalimisha kwa Mungu

Mistari 5 ya Biblia kuhusu Kujisalimisha kwa Mungu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Yakobo 4:7

Basi mtiini Mungu. Mpingeni ibilisi, naye atawakimbia.

02 Warumi 6:13

Wala msivitoe viungo vya miili yenu vitumike kama vyombo vya uovu vya kutenda dhambi, bali jitoeni kwa Mungu, kama watu waliotolewa kutoka mautini kuingia uzimani. Nanyi vitoeni viungo vya miili yenu kwake kama vyombo vya haki.

03 Yakobo 4:10

Jinyenyekezeni mbele za Bwana, naye atawainua.

04 1 Petro 5:6

Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake.

05 Warumi 12:1

Kwa hiyo, ndugu zangu, nawasihi kwa rehema zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu na inayompendeza Mungu, hii ndiyo ibada yenu yenye maana.

Mada zinazohusiana