Mistari ya Biblia Kuhusu Kushuhudia
Mistari 11 ya Biblia kuhusu Kushuhudia ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Lakini Roho Mtakatifu atakapowajia, mtapokea nguvu, nanyi mtanishuhudia huko Yerusalemu, kote Uyahudi na Samaria, hadi miisho ya dunia.”
Kwa upande wetu, hatuwezi kunyamaza kuhusu mambo tuliyoyaona na kuyasikia.”
Badala yake, katika mioyo yenu mkirini Kristo kuwa Bwana mtakatifu. Mwe tayari wakati wote kujitetea mbele ya yeyote anayewauliza sababu ya tumaini mlilo nalo.
Nanyi pia mnashuhudia kuhusu mimi, kwa sababu mmekuwa pamoja nami tangu mwanzo.
Vilevile, nuru yenu inapaswa kung’aa mahali ambapo watu wanaweza kuiona, ili waone matendo yenu mazuri na kumtukuza Baba yenu wa mbinguni.
Ukitangaza kwa kinywa chako kwamba Yesu ni Bwana, na ukaamini kwa moyo wako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, basi utaokolewa. Kwa maana watu huamini kwa moyo, na hilo huwaletea haki; hukiri kwa kinywa, na hilo huwaletea wokovu.
Nathanaeli akajibu, “Je, kitu chema kinaweza kutoka mahali kama Nazareti?” Filipo akamwambia, “Njoo uone.”
Utakuwa shahidi wake kwa watu wote, ukiwaeleza yale uliyoyaona na kuyasikia.
Njooni, sikilizeni, ninyi nyote mnaomcha Mungu; niwasimulie mambo yeye aliyonitendea.
Akajibu, “Kama yeye ni mwenye dhambi, sijui. Ninajua jambo moja: nilikuwa kipofu, na sasa ninaweza kuona.”
Lakini Yesu hakumruhusu, bali alimwambia, “Nenda nyumbani kwa watu wako, ukawajulishe yote ambayo Bwana amekutendea, na jinsi alivyokuonea huruma.”