Mistari ya Biblia Kuhusu Miguu Mizuri

Mistari 6 ya Biblia kuhusu Miguu Mizuri ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 6 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 Warumi 10:15 Mstari mkuu

Na watu watatangazaje ikiwa hawajatumwa? Kama ilivyoandikwa, “Miguu ya wale wanaoleta habari njema za mambo mema inapendeza kama nini!”

02 Warumi 10:14

Basi, watamwitaje ikiwa hawajamwamini? Na watamwaminije ikiwa hawajawahi kumsikia? Na watasikiaje bila mtu wa kutangaza?

03 Matendo 1:8

Lakini Roho Mtakatifu atakapowajia, mtapokea nguvu, nanyi mtanishuhudia huko Yerusalemu, kote Uyahudi na Samaria, hadi miisho ya dunia.”

04 Warumi 10:13

Kwa maana “wote watakaoliitia jina la Bwana wataokolewa.”

05 1 Wakorintho 9:16

Kuhubiri Injili hakunipi sababu ya kuona fahari, kwa maana nimelazimishwa kufanya hivyo. Ole wangu nisipohubiri Injili!

06 2 Wakorintho 5:20

Kwa hiyo sisi ni mabalozi tunaozungumza kwa niaba ya Kristo, na ni Mungu mwenyewe anayetoa wito wake kupitia sisi. Tukizungumza kwa niaba ya Kristo, tunawasihi: mpatanishwe na Mungu.

Mada zinazohusiana