Mistari ya Biblia Kuhusu Nenda Ukatangaze

Mistari 12 ya Biblia kuhusu Nenda Ukatangaze ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Marko 5:19

Yesu hakumruhusu, bali alimwambia, “Nenda nyumbani kwa jamaa yako ukawaeleze mambo makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokuhurumia.”

02 Zaburi 96:3

Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.

03 1 Nyakati 16:24

Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.

04 Yohana 4:28-29

Yule mwanamke akaacha mtungi wake, akarudi mjini akawaambia watu, “Njooni mkamwone mtu aliyeniambia kila kitu nilichotenda! Je, yawezekana huyu ndiye Kristo?”

05 Matendo 1:8

Lakini mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, Uyahudi kote na Samaria, hadi miisho ya dunia.”

06 Isaya 6:8

Kisha nikasikia sauti ya Bwana ikisema, “Nimtume nani? Ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu?” Nami nikasema, “Mimi hapa. Nitume mimi!”

07 Mathayo 28:19-20

Kwa sababu hii, enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika mimi niko pamoja nanyi siku zote, hadi mwisho wa nyakati.”

08 Marko 16:15

Akawaambia, “Enendeni ulimwenguni kote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

09 Luka 24:47

Toba na msamaha wa dhambi zitatangaziwa mataifa yote kupitia jina lake kuanzia Yerusalemu.

10 Matendo 5:20

“Nendeni, mkasimame Hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya uzima huu mpya.”

11 Yohana 1:41

Kitu cha kwanza Andrea alichofanya ni kumtafuta Simoni nduguye na kumwambia, “Tumemwona Masiya” (yaani, Kristo).

12 Zaburi 105:1

Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake, wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda.

Mada zinazohusiana