Mistari ya Biblia Kuhusu Karama ya Haki
Mistari 8 ya Biblia kuhusu Karama ya Haki ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Ikiwa kifo kilitawala kupitia mtu mmoja kwa sababu ya kosa la mtu huyo mmoja, ni hakika zaidi sana kwamba wale wanaopokea neema kwa kipimo kamili na zawadi ya haki watatawala katika uzima kupitia mtu yule mmoja, Yesu Kristo.
Basi, kama kosa moja lilileta adhabu kwa watu wote, vivyo hivyo tendo moja la haki linaleta kwa watu wote kuhesabiwa haki na kupewa uzima.
Lakini wanahesabiwa haki kama zawadi, bila malipo, kwa neema yake, kupitia ukombozi unaopatikana katika Kristo Yesu.
Ujira ambao dhambi hulipa ni kifo, lakini zawadi ya bure ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Kristo hakuwahi kujua dhambi, lakini kwa ajili yetu Mungu alimfanya kuwa dhambi, ili, tukiwa tumeunganishwa naye, sisi tufanyike haki ya Mungu.
ili, kama dhambi ilivyoshika utawala wake kupitia kifo, neema nayo itawale kupitia haki na kuongoza hadi uzima wa milele kupitia Yesu Kristo Bwana wetu.
na nionekane kuwa ndani yake, bila haki yangu mwenyewe inayotokana na kuishika sheria, bali nikiwa na haki inayopatikana kupitia imani katika Kristo: haki itokayo kwa Mungu, inayotegemea imani.
Daudi anasema vivyo hivyo anapozungumza juu ya furaha ya mtu ambaye Mungu anamhesabu kuwa mwenye haki bila matendo: