Mistari ya Biblia Kuhusu Kuhesabiwa Haki kwa Imani
Mistari 12 ya Biblia kuhusu Kuhesabiwa Haki kwa Imani ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Basi, kwa kuwa sasa tumehesabiwa haki kwa imani, tuna amani na Mungu kupitia Bwana wetu Yesu Kristo.
Lakini wanahesabiwa haki kama zawadi, bila malipo, kwa neema yake, kupitia ukombozi unaopatikana katika Kristo Yesu.
Hata hivyo tunajua kwamba hakuna mtu anayehesabiwa haki kwa matendo ya sheria; mtu huhesabiwa haki kwa njia ya imani katika Yesu Kristo tu. Kwa hiyo sisi pia tumemwamini Kristo Yesu, ili tuhesabiwe haki kwa imani katika Kristo wala si kwa matendo ya sheria, kwa sababu hakuna binadamu atakayehesabiwa haki kwa matendo ya sheria.
Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, ila anamwamini Mungu anayemhesabia haki mtu asiyemcha Mungu, imani hiyo inahesabiwa kuwa haki.
ili, tukiwa tumehesabiwa haki kwa neema yake, tuwe warithi wenye tumaini la uzima wa milele.
Kwa njia ya sheria hakuna mtu anayehesabiwa haki machoni pa Mungu; hilo ni wazi, kwa kuwa “Mtu aliye mwenye haki ataishi kwa imani.”
Yesu alitolewa afe kwa sababu ya makosa yetu, naye akafufuliwa ili sisi tupate kuhesabiwa haki.
kila anayeamini anaondolewa hatia kupitia yeye.
Kwa maana tuna hakika kwamba mtu anahesabiwa haki kwa imani, bila matendo ya sheria.
Kwa kuwa sasa tumehesabiwa haki kwa damu yake, ni hakika zaidi kwamba tutaokolewa kupitia yeye kutoka katika ghadhabu ya Mungu.
Kwa maana watu huamini kwa moyo, na hilo huwaletea haki; hukiri kwa kinywa, na hilo huwaletea wokovu.
na nionekane kuwa ndani yake, bila haki yangu mwenyewe inayotokana na kuishika sheria, bali nikiwa na haki inayopatikana kupitia imani katika Kristo: haki itokayo kwa Mungu, inayotegemea imani.