Mistari ya Biblia Kuhusu Kufanywa Wana
Mistari 9 ya Biblia kuhusu Kufanywa Wana ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
ili awakomboe watu walioishi chini ya sheria, nasi tufanywe wana.
Hamkupokea roho ya utumwa ambayo ingewarudisha tena chini ya hofu. Mlimpokea Roho wa kufanywa wana, na katika Roho tunaita, “Aba, Baba!”
Alitutenga tangu awali tufanywe wana wake kupitia Yesu Kristo. Ndivyo alivyopenda kufanya kwa moyo mkunjufu,
Lakini wote waliompokea, wale wanaoliamini jina lake, aliwapa mamlaka ya kuwa watoto wa Mungu.
Fikirini upendo mkuu ambao Baba ametupatia: tunaitwa watoto wa Mungu, na kweli sisi ni watoto wake. Sababu ya ulimwengu kutotujua ni kwamba haukumjua yeye.
Kwa maana katika Kristo Yesu ninyi nyote ni wana wa Mungu, kupitia imani.
ili neema yake yenye utukufu isifiwe, neema ambayo ametupa bure katika yule Mpendwa.
Wala si uumbaji peke yake. Sisi wenyewe, tulio na Roho kama sehemu ya kwanza ya mavuno, nasi tunaugua ndani yetu huku tukitamani kufanywa wana, mwili wetu utakapokombolewa.
“Nitakuwa Baba yenu, nanyi mtakuwa wana wangu na binti zangu,” asema Bwana Mwenyezi.