Mistari ya Biblia Kuhusu Kiasi
Mistari 14 ya Biblia kuhusu Kiasi ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
upole na kujitawala. Hakuna sheria inayopinga mambo kama haya.
Mtu asiyeweza kujizuia ni mji uliobomolewa, ulioachwa bila kuta.
Kila mshindani hujinyima mambo mengi katika mazoezi yake. Wao hukubali hivyo ili washinde shada linalonyauka upesi; sisi, ili tushinde shada lisilonyauka kamwe.
Inatufundisha kukataa maisha yasiyomcha Mungu na tamaa za ulimwengu, na kuishi maisha ya kiasi, ya haki na ya kumcha Mungu katika nyakati hizi za sasa,
ufahamu utoe kujitawala, kujitawala kutoe uvumilivu, uvumilivu utoe utauwa,
Uvumilivu ni bora kuliko nguvu za shujaa, na kujitawala ni bora kuliko kuuteka mji.
Kwa maana Mungu hakutupa roho ya hofu, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya akili timamu.
Badala yake, nauadhibu mwili wangu kwa mapigo na kuutendea kama mtumishi wangu, ili baada ya kuwahubiri wengine, mimi mwenyewe nisije nikaonekana sifai.
Fahamuni hili kwa hakika, ndugu zangu wapendwa. Kila mtu anapaswa kuwa tayari kusikiliza, kuchelewa kusema, na kuchelewa kukasirika,
Wale ambao ni wa Kristo wameigongomea msalabani asili ya dhambi, pamoja na mihemko yake na tamaa zake.
Kuweni na akili timamu. Kesheni. Ibilisi, mpinzani wenu, anazurura kama simba anayenguruma, akiwinda mtu wa kummeza.
Wapumbavu humwaga hasira yao yote, lakini wenye hekima huizuia kwa utulivu.
Basi tusilale kama wengine, bali tukae macho na kuwa makini.
Badala yake, jivikeni Bwana Yesu Kristo kama vazi, wala msifanye mipango ya kutimiza tamaa za asili ya dhambi.