Mistari ya Biblia Kuhusu Takeni Karama kwa Bidii

Mistari 11 ya Biblia kuhusu Takeni Karama kwa Bidii ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 1 Wakorintho 14:1

Fuateni upendo na kutaka sana karama za roho, hasa karama ya unabii.

02 1 Wakorintho 12:31

Basi tamanini sana karama zilizo kuu. Nami nitawaonyesha njia iliyo bora zaidi.

03 1 Wakorintho 14:12

Vivyo hivyo na ninyi. Kwa kuwa mnatamani kuwa na karama za rohoni, jitahidini kuzidi sana katika karama kwa ajili ya kulijenga kanisa.

04 1 Wakorintho 14:39

Kwa hiyo ndugu zangu, takeni sana kutoa unabii na msikataze watu kusema kwa lugha.

05 Warumi 12:11

Msiwe wavivu, bali mwe na bidii katika roho mkimtumikia Bwana.

06 1 Wakorintho 14:3

Lakini anayetoa unabii anasema na watu akiwajenga, kuwatia moyo na kuwafariji.

07 1 Wakorintho 14:5

Ningependa kila mmoja wenu anene kwa lugha lakini ningependa zaidi nyote mtoe unabii. Kwa kuwa yeye atoaye unabii ni mkuu kuliko anenaye kwa lugha, isipokuwa atafsiri, ili kanisa lipate kujengwa.

08 1 Wakorintho 14:40

Lakini kila kitu kitendeke kwa heshima na kwa utaratibu.

09 1 Wakorintho 14:26

Basi tuseme nini ndugu zangu? Mnapokutana pamoja, kila mmoja ana wimbo, au neno la mafundisho, au ufunuo, lugha mpya au atatafsiri. Mambo yote yatendeke kwa ajili ya kulijenga kanisa.

10 1 Timotheo 4:14

Usiache kutumia kipawa kilicho ndani yako, ambacho ulipewa kwa neno la unabii wakati wazee walikuwekea mikono.

11 2 Timotheo 1:6

Kwa sababu hii nakukumbusha uchochee ile karama ya Mungu, iliyowekwa ndani yako nilipokuwekea mikono yangu.

Mada zinazohusiana