Mistari ya Biblia Kuhusu Upendo Karama Iliyo Kuu

Mistari 15 ya Biblia kuhusu Upendo Karama Iliyo Kuu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 1 Wakorintho 13:13

Basi sasa, yanadumu mambo haya matatu: Imani, tumaini na upendo. Lakini lililo kuu miongoni mwa haya matatu ni upendo.

02 1 Wakorintho 13:1

Hata kama nitasema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa kengele inayolialia au toazi livumalo.

03 1 Wakorintho 13:2

Ningekuwa na karama ya unabii na kujua siri zote na maarifa yote, hata kama nina imani kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu.

04 1 Wakorintho 13:8

Upendo haushindwi kamwe. Lakini ukiwepo unabii, utakoma; zikiwepo lugha, zitakoma; yakiwepo maarifa, yatapita.

05 Wakolosai 3:14

Zaidi ya maadili haya yote jivikeni upendo, ambao ndio unaofunga kila kitu pamoja katika umoja mkamilifu.

Upendo huvumilia, upendo hufadhili, upendo hauoni wivu, hauna majivuno, hauna kiburi. Haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, haukasiriki upesi, hauweki kumbukumbu ya mabaya.

Upendo haufurahii mabaya bali hufurahi pamoja na kweli. Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote.

08 1 Yohana 4:8

Yeye asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu ni pendo.

09 Yohana 13:34-35

“Amri mpya nawapa: Mpendane kama mimi nilivyowapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi mpendane. Kama mkipendana ninyi kwa ninyi, kwa njia hii, watu wote watajua kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.”

10 Warumi 13:8

Msidaiwe kitu na mtu yeyote, isipokuwa kupendana, kwa maana yeye ampendaye mwenzake, ameitimiza sheria.

11 1 Yohana 4:16

Hivyo nasi twajua na kulitumainia pendo la Mungu alilo nalo kwa ajili yetu. Mungu ni Upendo. Kila akaaye katika upendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake.

12 1 Petro 4:8

Zaidi ya yote, dumuni katika upendo kwa maana upendo husitiri wingi wa dhambi.

13 Warumi 13:10

Upendo haumfanyii jirani jambo baya. Kwa hiyo upendo ndio utimilifu wa sheria.

14 1 Yohana 4:19

Twampenda yeye kwa sababu yeye alitupenda kwanza.

15 Wagalatia 5:6

Kwa maana ndani ya Kristo Yesu, kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuleti tofauti, bali lililo muhimu ni imani itendayo kazi kwa njia ya upendo.

Mada zinazohusiana