Mistari ya Biblia Kuhusu Karama Nyingi, Roho Mmoja

Mistari 11 ya Biblia kuhusu Karama Nyingi, Roho Mmoja ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 1 Wakorintho 12:4

Kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni yule yule.

Kuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana ni yule yule. Kisha kuna tofauti za kutenda kazi, lakini ni Mungu yule yule atendaye kazi zote kwa watu wote.

03 1 Wakorintho 12:11

Haya yote hufanywa na huyo huyo Roho mmoja, Roho naye humgawia kila mtu, kama apendavyo.

04 Waefeso 4:4

Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja.

05 Warumi 12:5

vivyo hivyo na sisi tulio wengi, tu mwili mmoja katika Kristo, nasi kila mmoja ni kiungo cha mwenzake.

06 1 Wakorintho 12:7

Basi kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa faida ya wote.

07 Waefeso 4:7

Lakini kila mmoja wetu amepewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa cha Kristo.

08 1 Wakorintho 12:14

Basi mwili si kiungo kimoja, bali ni viungo vingi.

09 Warumi 12:6

Tuna karama zilizotofautiana kila mmoja kutokana na neema tuliyopewa. Kama ni unabii na tutoe unabii kwa kadiri ya imani.

10 Waefeso 4:11

Ndiye aliweka wengine kuwa mitume, wengine kuwa manabii, wengine kuwa wainjilisti, wengine kuwa wachungaji na walimu,

11 1 Wakorintho 12:18

Lakini kama ilivyo, Mungu ameweka viungo katika mwili, kila kimoja kama alivyopenda.

Mada zinazohusiana