Mistari ya Biblia Kuhusu Nguvu Mpya

Mistari 13 ya Biblia kuhusu Nguvu Mpya ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Isaya 40:31

bali wale wamtumainio Bwana atafanya upya nguvu zao. Watapaa juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio wala hawatachoka, watatembea kwa miguu wala hawatazimia.

02 2 Wakorintho 4:16

Kwa hiyo, hatukati tamaa. Ingawa utu wetu wa nje unachakaa, utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.

03 Zaburi 103:5

atosheleza mahitaji yako kwa vitu vyema, ili ujana wako uhuishwe kama wa tai.

04 Wafilipi 4:13

Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

05 Isaya 40:29

Huwapa nguvu waliolegea na huongeza nguvu za wadhaifu.

06 Isaya 40:30-31

Hata vijana huchoka na kulegea, nao vijana wanaume hujikwaa na kuanguka, bali wale wamtumainio Bwana atafanya upya nguvu zao. Watapaa juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio wala hawatachoka, watatembea kwa miguu wala hawatazimia.

07 Zaburi 73:26

Mwili na moyo wangu vyaweza kushindwa, bali Mungu ni nguvu ya moyo wangu na fungu langu milele.

08 Waefeso 3:16

Namwomba Mungu awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyo yenu kwa njia ya Roho wake kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake,

09 Zaburi 28:7-8

Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu, moyo wangu umemtumaini yeye, nami nimesaidiwa. Moyo wangu unarukaruka kwa furaha nami nitamshukuru kwa wimbo. Bwana ni nguvu ya watu wake, ngome ya wokovu kwa mpakwa mafuta wake.

10 Nehemia 8:10

Nehemia akasema, “Nendeni mkafurahie chakula kizuri na vinywaji vitamu, na mpeleke sehemu kwa wale ambao hawana chochote cha kula. Siku hii ni takatifu kwa Bwana. Msihuzunike, kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu.”

11 Wakolosai 1:11

mkiwa mmetiwa nguvu kwa uwezo wote kwa kadiri ya nguvu yake yenye utukufu, ili mpate kuwa na wingi wa saburi na uvumilivu. Nanyi kwa furaha

12 Zaburi 138:3

Nilipoita, ulinijibu; ulinifanya jasiri na mwenye moyo hodari.

13 Habakuki 3:19

Bwana Mwenyezi ni nguvu yangu; huifanya miguu yangu kama miguu ya ayala, huniwezesha kupita juu ya vilima. Kwa kiongozi wa uimbaji. Kwa vinanda vyangu vya nyuzi.

Mada zinazohusiana