Mistari ya Biblia Kuhusu Kushikiliwa kwa Usalama

Mistari 8 ya Biblia kuhusu Kushikiliwa kwa Usalama ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Yohana 10:28

nami ninawapa uzima wa milele, hawataangamia kamwe wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka mikono yangu.

02 Yohana 10:29

Baba yangu aliyenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwapokonya kutoka mikononi mwake.

03 Warumi 8:38-39

Kwa maana nimekwisha kujua kwa hakika ya kuwa sio mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuja, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine chochote zitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu, Bwana wetu.

04 1 Petro 1:5

ninyi ambao mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani, hadi uje ule wokovu ulio tayari kufunuliwa nyakati za mwisho.

05 Yuda 1:24

Kwake yeye awezaye kuwalinda ninyi msianguke na kuwaleta mbele za utukufu wake mkuu bila dosari na kwa furaha ipitayo kiasi:

06 Kumbukumbu 33:27

Mungu wa milele ni kimbilio lako, na chini kuna mikono ya milele. Atamfukuza adui yako mbele yako, akisema, ‘Mwangamize yeye!’

07 Zaburi 37:24

ajapojikwaa, hataanguka, kwa maana Bwana humtegemeza kwa mkono wake.

08 Isaya 41:13

Kwa maana Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, nikushikaye mkono wako wa kuume na kukuambia, Usiwe na hofu, nitakusaidia.

Mada zinazohusiana