Mistari ya Biblia Kuhusu Tumaini katika Mungu

Mistari 12 ya Biblia kuhusu Tumaini katika Mungu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Zaburi 42:5

Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka? Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu? Weka tumaini lako kwa Mungu, kwa sababu bado nitamsifu, Mwokozi wangu na

02 Zaburi 42:11

Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka? Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu? Weka tumaini lako kwa Mungu, kwa sababu bado nitamsifu, Mwokozi wangu na Mungu wangu.

03 Zaburi 39:7

“Lakini sasa Bwana, nitafute nini? Tumaini langu ni kwako.

04 Maombolezo 3:24

Nimeiambia nafsi yangu, “ Bwana ni fungu langu, kwa hiyo nitamngojea.”

05 Zaburi 130:5

Namngojea Bwana, nafsi yangu inangojea, katika neno lake naweka tumaini langu.

06 Zaburi 33:20-22

Sisi tunamngojea Bwana kwa matumaini, yeye ni msaada wetu na ngao yetu. Mioyo yetu humshangilia, kwa maana tunalitumainia jina lake takatifu. Upendo wako usio na mwisho ukae juu yetu, Ee Bwana, tunapoliweka tumaini letu kwako.

07 Zaburi 71:5

Kwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee Bwana Mwenyezi, tegemeo langu tangu ujana wangu.

08 Zaburi 62:5

Ee nafsi yangu, upumzike, kwa Mungu peke yake, tumaini langu latoka kwake.

09 Mika 7:7

Lakini mimi, namtazama Bwana kwa matumaini, namngoja Mungu Mwokozi wangu; Mungu wangu atanisikia mimi.

10 Zaburi 147:11

Bwana hupendezwa na wale wamchao, wale wanaoweka tumaini lao katika upendo wake usiokoma.

11 Zaburi 33:18

Lakini macho ya Bwana yako kwa wale wamchao, kwa wale tumaini lao liko katika upendo wake usio na kikomo,

12 Warumi 15:13

Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha yote na amani katika kumwamini, ili mpate kujawa na tumaini tele kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Mada zinazohusiana

Kutoka kwa miongozo