Mistari ya Biblia Kuhusu Msimzimishe Roho

Mistari 11 ya Biblia kuhusu Msimzimishe Roho ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 11 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 1 Wathesalonike 5:19 Mstari mkuu

Msimfifishe Roho.

02 Waefeso 4:30

Na msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu. Ni kwa Roho huyo mlipigwa muhuri, mkawekwa alama kwa ajili ya siku ya ukombozi.

Msione unabii kuwa kitu duni. Pimeni kila jambo; shikilieni yaliyo mema;

04 Matendo 7:51

Jinsi mlivyo wakaidi! Mioyo yenu na masikio yenu hayajatahiriwa. Siku zote mnapigana na Roho Mtakatifu, nanyi mnafanya yale yale waliyofanya mababu zenu.

05 Wagalatia 5:25

Kwa kuwa uzima wetu unatoka kwa Roho, na tufuate uongozi wa Roho katika kila hatua tunayopiga.

06 Waebrania 3:7-8

Basi, kama Roho Mtakatifu asemavyo, “Leo, mkiisikia sauti yake, msiishupaze mioyo yenu kama ilivyotokea wakati wa uasi, siku ile ya majaribu jangwani,

07 Warumi 12:11

Bidii yenu isipungue kamwe; muwe na moto wa Roho; mtumikieni Bwana.

08 Zaburi 51:11

Usinifukuze mbali na uwepo wako, wala usimwondoe Roho wako Mtakatifu kwangu.

09 Waebrania 10:29

Basi mnadhani adhabu itakuwa mbaya zaidi kiasi gani kwa mtu aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, akaiona damu ya agano iliyomtakasa kuwa kitu cha kawaida tu, na kumdharau Roho wa neema?

10 Mathayo 12:31

Ndiyo sababu nawaambia kwamba watu wanaweza kusamehewa kila dhambi na kila kashfa, lakini hakuna atakayesamehewa kwa kumkufuru Roho.

11 Matendo 5:3

Petro alisema, “Anania, kwa nini Shetani ameujaza moyo wako hata ukamwongopea Roho Mtakatifu, ukajiwekea sehemu ya thamani ya kiwanja?

Mada zinazohusiana