Mistari ya Biblia Kuhusu Kuwapenda Ndugu

Mistari 14 ya Biblia kuhusu Kuwapenda Ndugu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 1 Yohana 4:20-21

Ikiwa mtu atasema, “Nampenda Mungu,” lakini anamchukia ndugu yake, yeye ni mwongo. Kwa maana kila mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, atampendaje Mungu asiyemuona? Naye ametupa amri hii: Yeyote anayempenda Mungu lazima pia ampende ndugu yake.

02 Yohana 13:34-35

“Amri mpya nawapa: Mpendane kama mimi nilivyowapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi mpendane. Kama mkipendana ninyi kwa ninyi, kwa njia hii, watu wote watajua kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.”

03 1 Yohana 3:16

Kwa namna hii twaweza kulijua pendo la Mungu: Kwa sababu Yesu Kristo aliutoa uhai wake kwa ajili yetu. Nasi imetupasa kuutoa uhai kwa ajili ya hao ndugu.

04 1 Petro 1:22

Basi kwa kuwa mmejitakasa nafsi zenu kwa kuitii ile kweli hata mkawa na upendo wa ndugu usio na unafiki, basi pendaneni kwa dhati kutoka moyoni.

05 Warumi 12:10

Pendaneni ninyi kwa ninyi kwa upendo wa ndugu. Waheshimuni na kuwatanguliza wengine.

06 1 Yohana 3:14

Sisi tunajua ya kwamba tumepita mautini kuingia uzimani, kwa sababu tunawapenda ndugu. Kila asiyempenda ndugu yake akaa mautini.

07 1 Yohana 4:7-8

Wapendwa, tupendane, kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu. Kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. Yeye asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu ni pendo.

08 1 Yohana 4:11

Marafiki wapendwa, kama Mungu alivyotupenda sisi, imetupasa na sisi kupendana.

09 Waebrania 13:1

Endeleeni kupendana kama ndugu.

10 1 Yohana 3:18

Watoto wapendwa, tusipende kwa maneno au kwa ulimi bali kwa tendo na kweli.

11 Yohana 13:34

“Amri mpya nawapa: Mpendane kama mimi nilivyowapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi mpendane.

Sasa kuhusu upendo wa ndugu hamna haja mtu yeyote kuwaandikia, kwa maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.

13 Wagalatia 5:13

Ndugu zangu, ninyi mliitwa ili mwe huru, hivyo msitumie uhuru wenu kama fursa ya kufuata tamaa za mwili, bali tumikianeni ninyi kwa ninyi kwa upendo.

14 1 Yohana 3:23

Hii ndiyo amri yake: kwamba tuliamini Jina la Mwanawe, Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi kama yeye alivyotuamuru.

Mada zinazohusiana