Mistari ya Biblia Kuhusu Inueni Mikono Yenu
Mistari 11 ya Biblia kuhusu Inueni Mikono Yenu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Inueni mikono yenu kuelekea mahali patakatifu, mkambariki BWANA!
Hivyo nitakubariki wewe maisha yangu yote; nitainua mikono yangu nikiliitia jina lako.
Kwa hiyo nataka wanaume kila mahali waombe, wakiinua mikono mitakatifu, bila hasira wala ugomvi.
Maombi yangu na yasimame mbele yako kama uvumba, mikono yangu iliyoinuliwa kama sadaka ya jioni.
Usikilize sauti yangu ninapoomba rehema na kukulilia unisaidie, ninapoinua mikono yangu kuelekea chumba cha ndani kabisa cha nyumba yako takatifu.
Macho yangu yamechoka kwa huzuni. Siku baada ya siku ninakuita, Ee BWANA, nikikunyooshea mikono yangu.
Nitainua mikono yangu kuelekea amri zako, ambazo ninazipenda, nami nitazitafakari kanuni zako.
Ninakunyooshea mikono yangu; nafsi yangu yote inakungoja kama ardhi iliyochoshwa na ukame. Sela
Kila Musa alipoushikilia mkono wake juu, Israeli walishinda; na kila alipoushusha, Amaleki walishinda.
Enyi mataifa yote, pigeni makofi! Mpazieni Mungu sauti kwa vigelegele vya furaha!
Kisha Sulemani akasimama mbele ya madhabahu ya BWANA, mbele ya kusanyiko lote la Israeli, akainyoosha mikono yake kuelekea mbinguni.