Mistari ya Biblia Kuhusu Kuongozwa na Roho

Mistari 15 ya Biblia kuhusu Kuongozwa na Roho ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Warumi 8:14

Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio watoto wa Mungu.

02 Warumi 8:16

Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu ya kwamba sisi tu watoto wa Mungu.

03 Wagalatia 5:18

Lakini kama mkiongozwa na Roho, hamko chini ya sheria.

04 Yohana 16:13

Atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie katika kweli yote. Yeye hatanena kwa ajili yake mwenyewe, bali atanena yale yote atakayosikia, naye atawaonyesha mambo yajayo.

05 Zaburi 143:10

Nifundishe kufanya mapenzi yako, kwa maana wewe ndiwe Mungu wangu, Roho wako mwema na aniongoze katika nchi tambarare.

06 Wagalatia 5:25

Kwa kuwa tunaishi kwa Roho, basi, tuenende kwa Roho.

07 Isaya 30:21

Mkigeuka kuume au kushoto, masikio yenu yatasikia sauti nyuma yenu ikisema, “Hii ndiyo njia, ifuateni.”

08 Warumi 8:4

ili kwamba haki ipatikanayo kwa sheria itimizwe ndani yetu sisi, ambao hatuenendi kwa kuufuata mwili bali kwa kufuata Roho.

09 Zaburi 25:4-5

Nionyeshe njia zako, Ee Bwana, nifundishe mapito yako, niongoze katika kweli yako na kunifundisha, kwa maana wewe ni Mungu Mwokozi wangu, nalo tumaini langu liko kwako wakati wote.

10 Warumi 8:5-6

Kwa maana wale wanaoishi kwa kuufuata mwili huziweka nia zao katika vitu vya mwili, lakini wale wanaoishi kwa kufuata Roho, huziweka nia zao katika mambo ya Roho. Kwa maana kuwa na nia ya mwili ni mauti, bali kuwa na nia inayoongozwa na Roho ni uzima na amani.

11 Matendo 8:29

Roho Mtakatifu akamwambia Filipo, “Nenda kwenye lile gari ukae karibu nalo.”

12 Matendo 13:2

Walipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, “Nitengeeni Sauli na Barnaba kwa kazi ile maalum niliyowaitia.”

13 Matendo 16:6-7

Paulo pamoja na wenzake wakasafiri sehemu za Frigia na Galatia, kwa kuwa Roho Mtakatifu hakuwaruhusu kulihubiri neno huko Asia. Walipofika mpaka wa Misia, wakajaribu kuingia Bithinia lakini Roho wa Yesu hakuwaruhusu.

14 Mithali 3:5-6

Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako.

15 Zaburi 32:8

Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; nitakushauri na kukuangalia.

Mada zinazohusiana