Mistari ya Biblia Kuhusu Roho Ndani Yetu
Mistari 6 ya Biblia kuhusu Roho Ndani Yetu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Je, hamjui kwamba ninyi kwa pamoja ni hekalu la Mungu, na kwamba Roho wa Mungu anaishi kati yenu?
Au hamjui kwamba mwili wenu ni hekalu ambamo Roho Mtakatifu anaishi, Roho aliye ndani yenu, ambaye Mungu amewapa? Ninyi si wenu wenyewe.
Lakini ninyi hamko chini ya utawala wa asili ya dhambi; mko chini ya utawala wa Roho, ikiwa kweli Roho wa Mungu amefanya makao ndani yenu. Ikiwa mtu hana Roho wa Kristo, mtu huyo si wake.
Ilinde hazina nzuri uliyokabidhiwa, kwa msaada wa Roho Mtakatifu anayekaa ndani yetu.
Hivi ndivyo tunavyojua kwamba tunakaa ndani yake na yeye anakaa ndani yetu: ametupa kutoka kwa Roho wake mwenyewe.
Na kwa kuwa ninyi ni wana, Mungu amemtuma Roho wa Mwana wake aingie mioyoni mwetu, naye Roho anaita, “Aba, Baba!”