Mistari ya Biblia Kuhusu Kuenenda kwa Roho

Mistari 10 ya Biblia kuhusu Kuenenda kwa Roho ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Wagalatia 5:25

Kwa kuwa tunaishi kwa Roho, basi, tuenende kwa Roho.

02 Wagalatia 5:16

Kwa hiyo nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.

03 Warumi 8:4

ili kwamba haki ipatikanayo kwa sheria itimizwe ndani yetu sisi, ambao hatuenendi kwa kuufuata mwili bali kwa kufuata Roho.

04 Wagalatia 5:22-23

Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi. Katika mambo kama haya hakuna sheria.

05 Warumi 8:1

Kwa hiyo, sasa hakuna hukumu ya adhabu kwa wale walio ndani ya Kristo Yesu, wale ambao hawaenendi kwa kuufuata mwili bali kwa kufuata Roho.

06 Warumi 8:5

Kwa maana wale wanaoishi kwa kuufuata mwili huziweka nia zao katika vitu vya mwili, lakini wale wanaoishi kwa kufuata Roho, huziweka nia zao katika mambo ya Roho.

07 Warumi 8:13-14

kwa maana mkiishi kwa kuufuata mwili, mtakufa, lakini kama mkiyaua matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio watoto wa Mungu.

08 Wagalatia 5:18

Lakini kama mkiongozwa na Roho, hamko chini ya sheria.

09 Wagalatia 6:8

Apandaye kwa mwili, katika mwili wake atavuna uharibifu, lakini yeye apandaye katika Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.

10 Waefeso 5:8-9

Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, lakini sasa ninyi ni nuru katika Bwana. Enendeni kama watoto wa nuru (kwa kuwa tunda la nuru hupatikana katika wema wote, haki na kweli),

Mada zinazohusiana