Mistari ya Biblia Kuhusu Uvivu
Mistari 9 ya Biblia kuhusu Uvivu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Ewe mvivu, mwendee mchwa; zitafakari njia zake ukapate hekima!
Mvivu hutamani sana na hapati kitu, bali nafsi ya mwenye bidii hutoshelezwa kikamilifu.
Mvivu halimi kwa majira; kwa hiyo wakati wa mavuno hutazama lakini hapati chochote.
Nilipita karibu na shamba la mvivu, karibu na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili, miiba ilikuwa imeota kila mahali, ardhi ilikuwa imefunikwa na magugu, na ukuta wa mawe ulikuwa umebomoka.
Kwa maana hata tulipokuwa pamoja nanyi, tuliwapa amri kwamba: “Mtu yeyote asiyetaka kufanya kazi, hata kula asile.”
Uvivu huleta usingizi mzito, naye mtu mzembe huona njaa.
Kama vile mlango ugeukavyo kwenye bawaba zake, ndivyo mvivu ajigeuzavyo kitandani mwake.
Kutamani sana kwa mvivu kutakuwa kifo chake, kwa sababu mikono yake haitaki kufanya kazi.
Kama mtu ni mvivu paa la nyumba huinama, kutokana na mikono milegevu, nyumba huvuja.