Mistari ya Biblia Kuhusu Chuma Hunoa Chuma

Mistari 8 ya Biblia kuhusu Chuma Hunoa Chuma ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Mithali 27:17

Kama vile chuma kinoavyo chuma, ndivyo mtu amnoavyo mwenzake.

02 Mithali 27:6

Majeraha kutoka kwa rafiki yaonyesha uaminifu, bali kubusu kwa adui ni kwingi sana.

03 Mithali 27:9

Manukato na uvumba huleta furaha moyoni, nao uzuri wa rafiki huchipuka kutoka kwenye ushauri wake wa uaminifu.

04 Waebrania 10:24

Tuangaliane na kuhimizana sisi kwa sisi katika upendo na katika kutenda mema.

05 Mhubiri 4:9-10

Wawili ni afadhali kuliko mmoja, kwa sababu wana malipo mazuri kwa kazi yao: Kama mmoja akianguka, mwenzake atamwinua. Lakini ni jambo la kuhuzunisha kwa mtu yule aangukaye naye hana wa kumwinua!

06 Mithali 13:20

Yeye atembeaye na mwenye hekima atapata hekima, bali rafiki wa mpumbavu hupata madhara.

07 Mhubiri 4:12

Ingawa mtu mmoja aweza kushindwa, watu wawili wanaweza kumkabili adui na kumshinda. Kamba ya nyuzi tatu haikatiki kwa urahisi.

08 Wakolosai 3:16

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu, mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, huku mkiwa na shukrani mioyoni mwenu.

Mada zinazohusiana