Mistari ya Biblia Kuhusu Uadilifu

Mistari 15 ya Biblia kuhusu Uadilifu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Mithali 10:9

Mtu mwadilifu hutembea salama, lakini mtu aendaye katika njia zilizopotoka atagunduliwa.

02 Mithali 11:3

Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao.

03 Zaburi 25:21

Uadilifu na uaminifu vinilinde, kwa sababu tumaini langu ni kwako.

04 Ayubu 27:5

Sitakubaliana nanyi kabisa kuwa mko sahihi; hadi nife, sitakana uadilifu wangu.

05 Mithali 20:7

Mtu mwenye haki huishi maisha yasiyo na lawama, wamebarikiwa watoto wake baada yake.

06 Zaburi 26:1

Ee Bwana, nithibitishe katika haki, maana nimeishi maisha yasiyo na lawama; nimemtumainia Bwana bila kusitasita.

07 Mithali 19:1

Afadhali mtu maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama, kuliko mpumbavu ambaye midomo yake imepotoka.

08 Mithali 28:6

Afadhali maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama kuliko tajiri ambaye njia zake ni potovu.

09 Zaburi 41:12

Katika uadilifu wangu unanitegemeza na kuniweka kwenye uwepo wako milele.

10 1 Nyakati 29:17

Ninajua, Mungu wangu, kwamba wewe huujaribu moyo na unapendezwa na unyofu. Vitu hivi vyote nimetoa kwa hiari na kwa moyo mnyofu. Nami sasa nimeona kwa furaha jinsi watu wako walioko hapa kwa hiari yao walivyokutolea wewe.

11 Mithali 11:1

Bwana huchukia sana mizani za udanganyifu, bali vipimo sahihi ni furaha yake.

12 Tito 2:7

Katika kila jambo uwe kielelezo kwa kutenda mema. Katika mafundisho yako uonyeshe uadilifu, utaratibu,

13 Luka 16:10

“Yeyote aliye mwaminifu katika mambo madogo, pia ni mwaminifu hata katika mambo makubwa, naye mtu ambaye si mwaminifu katika mambo madogo pia si mwaminifu katika mambo makubwa.

14 Mithali 21:3

Kufanya yaliyo sawa na haki inakubalika zaidi kwa Bwana kuliko dhabihu.

15 Zaburi 78:72

Naye Daudi aliwachunga kwa uadilifu wa moyo, kwa mikono ya ustadi aliwaongoza.

Mada zinazohusiana