Mistari ya Biblia Kuhusu Uaminifu
Mistari 12 ya Biblia kuhusu Uaminifu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
BWANA huichukia midomo ya uongo, bali watu waaminifu ni furaha yake.
BWANA huchukia mizani ya udanganyifu, bali uzito wa haki humpendeza.
Basi sasa kwa kuwa mmeuvua uongo, kila mmoja wenu amwambie jirani yake kweli, kwa maana sisi kwa sisi ni viungo.
Tunajali yaliyo ya heshima, mbele za Bwana na mbele za watu pia.
Wafalme hufurahia maneno ya kweli; humthamini anayesema yaliyo sawa.
Msiseme uongo ninyi kwa ninyi. Mmeuvua utu wa zamani pamoja na mienendo yake,
Afadhali kuwa maskini na kuishi kwa uadilifu kuliko kuwa mpumbavu mwenye ulimi wa uongo.
Msiache kutuombea. Tuna hakika kwamba dhamiri yetu ni safi, kwa kuwa tunataka kuishi ipasavyo kwa kila namna.
Kutoa jibu lililo wazi ni kama kubusu midomo.
Msimrudishie mtu yeyote uovu kwa uovu aliowatendea. Pangeni mapema kutenda yale ambayo kila mtu anayatambua kuwa mema.
BWANA huchukia mawe mawili tofauti ya kupimia; mizani ya kudanganya ni mbaya.
Uuzuie ulimi wako usiseme mabaya, na midomo yako isiseme chochote cha uongo.