Mistari ya Biblia Kuhusu Kuenenda kwa Unyofu

Mistari 15 ya Biblia kuhusu Kuenenda kwa Unyofu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Zaburi 84:11

Kwa kuwa Bwana ni jua na ngao, Bwana hutoa wema na heshima; hakuna kitu chema anachowanyima wale ambao hawana hatia.

02 Zaburi 15:1-2

Bwana, ni nani awezaye kukaa katika Hekalu lako? Nani awezaye kuishi katika mlima wako mtakatifu? Ni yule aendaye pasipo mawaa, atendaye yaliyo haki, asemaye kweli toka moyoni mwake,

03 Mithali 2:7

Anahifadhi ushindi kwa ajili ya mwadilifu, yeye ni ngao kwa wale wasio na lawama,

04 Mithali 28:18

Yeye ambaye mwenendo wake hauna lawama hulindwa salama, bali yeye ambaye njia zake ni potovu ataanguka ghafula.

05 Mika 6:8

Amekuonyesha yaliyo mema, ee mwanadamu. Bwana anataka nini kwako? Ila kutenda kwa haki na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako.

06 Mithali 10:9

Mtu mwadilifu hutembea salama, lakini mtu aendaye katika njia zilizopotoka atagunduliwa.

07 Zaburi 1:1

Heri mtu yule ambaye haendi katika shauri la watu waovu, wala hasimami katika njia ya wenye dhambi, au kuketi katika baraza la wenye mizaha.

08 Mithali 11:3

Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao.

09 Zaburi 119:1

Heri wale walio waadilifu katika njia zao, wanaoenenda katika sheria ya Bwana.

10 Mithali 14:2

Yeye ambaye njia zake ni nyofu humcha Bwana, bali yeye ambaye njia zake zimepotoka humdharau Mungu.

11 Zaburi 37:37

Watafakari watu wasio na hatia, wachunguze watu wakamilifu, kuna mafanikio kwa mtu apendaye amani.

12 Isaya 33:15-16

Yeye aendaye kwa uadilifu na kusema lililo haki, yeye anayekataa faida ipatikanayo kwa dhuluma na kuizuia mikono yake isipokee rushwa, yeye azuiaye masikio yake dhidi ya mashauri ya mauaji, na yeye afumbaye macho yake yasitazame sana uovu: huyu ndiye mtu atakayeishi mahali pa juu, ambaye kimbilio lake litakuwa ngome ya mlimani. Atapewa mkate wake, na maji yake hayatakoma.

13 Mithali 20:7

Mtu mwenye haki huishi maisha yasiyo na lawama, wamebarikiwa watoto wake baada yake.

14 Mithali 13:6

Haki humlinda mtu mwadilifu, bali uovu humwangusha mwenye dhambi.

15 1 Yohana 1:7

Lakini tukienenda nuruni, kama yeye alivyo nuruni, twashirikiana sisi kwa sisi na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.

Mada zinazohusiana