Mistari ya Biblia Kuhusu Kuikimbia Dhambi

Mistari 12 ya Biblia kuhusu Kuikimbia Dhambi ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 2 Timotheo 2:22

Zikimbie tamaa mbaya za ujana, ufuate haki, imani, upendo na amani pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.

02 1 Wakorintho 6:18

Ikimbieni zinaa. Dhambi zingine zote atendazo mtu ziko nje ya mwili wake, lakini yeye aziniye hutenda dhambi ndani ya mwili wake mwenyewe.

03 1 Wakorintho 10:14

Kwa hiyo wapenzi wangu, zikimbieni ibada za sanamu.

04 1 Timotheo 6:11

Lakini wewe, mtu wa Mungu, yakimbie mambo haya yote. Fuata haki, utauwa, imani, upendo, saburi na upole.

05 Mwanzo 39:12

Mke wa Potifa akashika vazi Yosefu alilokuwa amevaa, akamwambia, “Njoo tukutane kimwili!” Lakini Yosefu akaacha vazi lake mkononi mwa huyo mwanamke, akatoka nje ya nyumba akikimbia.

06 Mithali 4:14-15

Usiuweke mguu wako katika njia ya waovu wala usitembee katika njia ya watu wabaya. Epukana nayo, usisafiri katika njia hiyo; achana nayo, na uelekee njia yako.

Jiepusheni na uovu wa kila namna.

08 2 Timotheo 2:19

Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, ukiwa na muhuri wenye maandishi haya: “Bwana anawajua walio wake”; tena, “Kila alitajaye jina la Bwana, na auache uovu.”

09 Yakobo 4:7

Basi mtiini Mungu. Mpingeni ibilisi, naye atawakimbia.

10 Mithali 5:8

Njia zenu ziwe mbali naye, msiende karibu na mlango wa nyumba yake,

11 Warumi 13:14

Bali jivikeni Bwana Yesu Kristo, wala msifikiri jinsi mtakavyotimiza tamaa za miili yenu yenye asili ya dhambi.

12 1 Petro 2:11

Wapenzi, ninawasihi, mkiwa kama wageni na wapitaji hapa ulimwenguni, epukeni tamaa mbaya za mwili ambazo hupigana vita na roho zenu.

Mada zinazohusiana