Mistari ya Biblia Kuhusu Kiburi
Mistari 13 ya Biblia kuhusu Kiburi ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Kiburi hutangulia maangamizi, roho ya majivuno hutangulia maanguko.
Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu, bali unyenyekevu huja na hekima.
Lakini yeye hutupatia neema zaidi. Hii ndiyo sababu Andiko husema: “Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.”
Bwana huwachukia sana wote wenye kiburi cha moyo. Uwe na hakika kwa hili: Hawataepuka kuadhibiwa.
Vivyo hivyo, ninyi mlio vijana watiini wazee. Nanyi nyote imewapasa kujivika unyenyekevu kila mtu kwa mwenzake, kwa kuwa, “Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.”
Kumcha Bwana ni kuchukia uovu; ninachukia kiburi na majivuno, tabia mbaya na mazungumzo potovu.
Kabla ya anguko moyo wa mtu hujaa kiburi, bali unyenyekevu hutangulia heshima.
Kiburi cha mtu humshusha, bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu hupata heshima.
Macho ya mtu mwenye majivuno yatanyenyekezwa na kiburi cha wanadamu kitashushwa, Bwana peke yake ndiye atakayetukuzwa siku hiyo.
Kwa maana kila mtu ajikwezaye atashushwa, naye ajishushaye atakwezwa.”
Kama mtu yeyote akijiona kuwa yeye ni bora na kumbe sivyo, basi mtu huyo anajidanganya mwenyewe.
Kwa ajili ya neema niliyopewa nawaambia kila mmoja miongoni mwenu, asijidhanie kuwa bora kuliko impasavyo, bali afikiri kwa busara kwa kulingana na kipimo cha imani Mungu aliyompa.
Huwadhihaki wale wanaodhihaki, lakini huwapa neema wale wanyenyekevu.