Mistari ya Biblia Kuhusu Mauti Imeshindwa
Mistari 13 ya Biblia kuhusu Mauti Imeshindwa ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
na sasa imedhihirishwa kwa kuonekana kwa Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Yeye ameiangamiza mauti, na kupitia Injili ameleta nuruni uzima na kutoharibika.
Adui wa mwisho atakayekomeshwa ni kifo.
Basi, kwa kuwa watoto wanashiriki maisha ya pamoja ya mwili na damu, yeye mwenyewe aliyapokea maisha hayo hayo kwa namna ile ile, ili kwa kifo chake amnyang’anye nguvu yule anayeshika mamlaka ya kifo, yaani Ibilisi, na kuwaweka huru wale ambao hofu ya kifo iliwaweka utumwani maisha yao yote.
Kila chozi atalifuta kutoka machoni mwao. Kifo hakitakuwapo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu. Mambo ya zamani yamepita.”
Mwili huu unaoharibika utakapokuwa umevaa kutoharibika, na mwili huu unaokufa utakapokuwa umevaa kutokufa, ndipo maneno yaliyoandikwa katika Maandiko yatatimia: “Kifo kimemezwa katika ushindi.” Kifo, ushindi wako uko wapi? Kifo, mwiba wako uko wapi?
Yesu akamwambia, “Mimi ni ufufuo na uzima. Wanaoniamini, hata wakifa, wataishi,
Kwa maana tunajua kwamba Kristo, kwa kuwa amefufuliwa kutoka kwa wafu, hatakufa tena; kifo si bwana wake tena.
Kwa maana nina hakika kabisa kwamba si kifo wala uzima, si malaika wala watawala, si mambo yaliyopo sasa wala yale yatakayokuja, si nguvu zozote, si vilivyo juu sana wala vilivyo chini kabisa, wala kitu kingine chochote kilichoumbwa: hakuna kitakachoweza kutukatilia mbali na upendo wa Mungu, ambao ni wetu katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Kweli kweli nawaambia, yeyote anayesikia neno langu na kumwamini aliyenituma ana uzima wa milele. Mtu huyo hahukumiwi, bali amekwisha toka kifoni na kuingia uzimani.
Lakini Mungu atalipa fidia kwa ajili ya uhai wangu na kuuweka huru kutoka makucha ya Kuzimu, kwa maana yeye atanichukua. Sela
Lakini Mungu ashukuriwe, kwa maana yeye hutupa ushindi kupitia Bwana wetu Yesu Kristo.
Kisha Kifo na Kuzimu vyenyewe vikatupwa ndani ya ziwa la moto. Ziwa la moto ndilo kifo cha pili.
Kweli kweli nawaambia, mtu yeyote akilishika neno langu, hataona kifo kamwe.”