Mistari ya Biblia Kuhusu Malimbuko
Mistari 15 ya Biblia kuhusu Malimbuko ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Lakini kila mmoja ana nafasi yake katika mpangilio: kwanza Kristo, malimbuko; baadaye, wakati wa kuja kwake, wale walio wake.
Lakini kwa kweli Kristo amefufuliwa kutoka kwa wafu. Yeye ni malimbuko ya wale waliofariki.
Na ikiwa Roho wa yule aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu amefanya makao ndani yenu, basi Mungu, aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu, ataipa uzima pia miili yenu inayokufa, kwa sababu Roho wake anaishi ndani yenu.
Yeye pia ni kichwa cha mwili, yaani kanisa. Yeye ndiye mwanzo, wa kwanza kuzaliwa kutoka miongoni mwa wafu, ili awe na nafasi ya kwanza katika kila kitu.
Tunaamini kwamba Yesu alikufa na akafufuka; vivyo hivyo, kupitia Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye wale ambao wamelala.
Kama vile wote walio wa Adamu wanakufa, vivyo hivyo wote walio wa Kristo watafanywa hai.
kwamba Kristo lazima ateswe, na kwamba, akiwa wa kwanza kufufuka kutoka kwa wafu, yeye angetangaza nuru kwa watu wetu wenyewe na kwa watu wa mataifa.”
na kutoka kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, na mtawala juu ya wafalme wa dunia. Kwa yeye anayetupenda, na aliyetuweka huru mbali na dhambi zetu kwa damu yake,
Ilikuwa ni mapenzi yake kutuzaa kupitia neno la kweli, ili tuwe kitu kama limbuko miongoni mwa viumbe vyake vyote.
Wala si uumbaji peke yake. Sisi wenyewe, tulio na Roho kama sehemu ya kwanza ya mavuno, nasi tunaugua ndani yetu huku tukitamani kufanywa wana, mwili wetu utakapokombolewa.
Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Kwa rehema yake kuu ametupa kuzaliwa upya. Kupitia kufufuka kwa Yesu Kristo kutoka kwa wafu ametuleta katika tumaini lenye uzima,
Kweli kweli nawaambia, punje ya ngano isipoanguka ardhini na kufa, inabaki punje moja tu; lakini ikifa, inazaa matunda mengi.
Kwa kuwa kifo kilikuja kupitia mwanadamu, ufufuo wa wafu nao unakuja kupitia mwanadamu.
Mwana ni sura ya Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza aliye juu ya viumbe vyote.
na ndiye aliye hai. Nilikuwa nimekufa, na tazama, niko hai milele na milele, na funguo za kifo na za Kuzimu ni zangu.