Mistari ya Biblia Kuhusu Kaburi Tupu

Mistari 5 ya Biblia kuhusu Kaburi Tupu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Luka 24:6

Hayuko hapa; amefufuka! Kumbukeni alivyowaambia alipokuwa bado yuko pamoja nanyi huko Galilaya kwamba:

02 Mathayo 28:6

Hayupo hapa, kwa kuwa amefufuka, kama vile alivyosema. Njooni mpatazame mahali alipokuwa amelazwa.

03 Marko 16:6

Yule malaika akawaambia, “Msistaajabu. Mnamtafuta Yesu, Mnazareti, aliyesulubiwa. Amefufuka! Hayuko hapa. Tazameni mahali walipomlaza.

04 Yohana 20:6-7

Ndipo Simoni Petro akaja, akimfuata nyuma akaenda moja kwa moja hadi ndani ya kaburi. Naye akaona vile vitambaa vya ile sanda vikiwa pale chini na kile kitambaa kilichokuwa kichwani mwa Yesu. Kitambaa hicho kilikuwa kimekunjwa mahali pa peke yake, mbali na vile vitambaa vya kitani vya ile sanda.

05 1 Wakorintho 15:4

ya kuwa alizikwa na alifufuliwa siku ya tatu, kama yasemavyo Maandiko,

Mada zinazohusiana