Mistari ya Biblia Kuhusu Zaidi ya Yote, Vaeni Upendo

Mistari 6 ya Biblia kuhusu Zaidi ya Yote, Vaeni Upendo ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Wakolosai 3:14

Zaidi ya maadili haya yote jivikeni upendo, ambao ndio unaofunga kila kitu pamoja katika umoja mkamilifu.

02 1 Wakorintho 13:13

Basi sasa, yanadumu mambo haya matatu: Imani, tumaini na upendo. Lakini lililo kuu miongoni mwa haya matatu ni upendo.

03 Wakolosai 3:12

Kwa hiyo, kwa kuwa ninyi mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao sana, jivikeni moyo wa huruma, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.

04 1 Petro 4:8

Zaidi ya yote, dumuni katika upendo kwa maana upendo husitiri wingi wa dhambi.

05 Warumi 13:8

Msidaiwe kitu na mtu yeyote, isipokuwa kupendana, kwa maana yeye ampendaye mwenzake, ameitimiza sheria.

06 1 Wakorintho 16:14

Fanyeni kila kitu katika upendo.

Mada zinazohusiana