Mistari ya Biblia Kuhusu Kuenenda katika Njia Zake

Mistari 5 ya Biblia kuhusu Kuenenda katika Njia Zake ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Kumbukumbu 10:12

Na sasa, ee Israeli, Bwana Mungu wako anataka nini kwako ila kumcha Bwana Mungu wako, kwenda katika njia zake, kumpenda na kumtumikia Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote,

02 Mika 6:8

Amekuonyesha yaliyo mema, ee mwanadamu. Bwana anataka nini kwako? Ila kutenda kwa haki na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako.

03 Zaburi 119:1-2

Heri wale walio waadilifu katika njia zao, wanaoenenda katika sheria ya Bwana. Heri wale wanaozishika shuhuda zake, wamtafutao kwa moyo wao wote.

04 Isaya 30:21

Mkigeuka kuume au kushoto, masikio yenu yatasikia sauti nyuma yenu ikisema, “Hii ndiyo njia, ifuateni.”

05 Wagalatia 5:25

Kwa kuwa tunaishi kwa Roho, basi, tuenende kwa Roho.

Mada zinazohusiana