Mistari ya Biblia Kuhusu Kuutumaini Uongozi Wake
Mistari 9 ya Biblia kuhusu Kuutumaini Uongozi Wake ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Moyo wa mtu huifikiri njia yake, bali Bwana huelekeza hatua zake.
Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako.
Mkabidhi Bwana njia yako, mtumaini yeye, naye atatenda hili:
Ninajua, Ee Bwana, kwamba maisha ya mwanadamu si yake mwenyewe; hawezi kuziongoza hatua zake mwenyewe.
Utamlinda katika amani kamilifu yeye ambaye moyo wake ni thabiti kwa sababu anakutumaini wewe.
Wakati ninapoogopa, nitakutumaini wewe. Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu, katika Mungu ninatumaini; sitaogopa. Mwanadamu apatikanaye na kufa, atanitenda nini?
Bwana ni Mwema, kimbilio wakati wa taabu. Huwatunza wale wanaomtegemea,
Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe, kwa maana wewe Bwana, hujawaacha kamwe wakutafutao.
Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako. Nitakutia nguvu na kukusaidia; nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu.