Mistari ya Biblia Kuhusu Enzi na Maongozi ya Mungu
Hakuna kilicho nje ya utawala wa Mungu; yeye hutenda mambo yote kwa kudira ya mapenzi yake. Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema. Aya hizi zinautuliza moyo katika udhibiti wa Mungu wenye hekima na upendo juu ya kila jambo dogo la maisha.
Bwana ameweka imara kiti chake cha enzi mbinguni, ufalme wake unatawala juu ya vyote.
Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu,” asema Bwana, “ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo.
Nasi tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote wampendao, katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.
Kuna wakati kwa ajili ya kila jambo, nayo majira kwa kila tendo chini ya mbingu:
Moyo wa mtu huifikiri njia yake, bali Bwana huelekeza hatua zake.
Bwana anatawala, amejivika utukufu; Bwana amejivika utukufu tena amejivika nguvu. Dunia imewekwa imara, haitaondoshwa.
Lakini, Ee Bwana, wewe ndiwe Baba yetu. Sisi ni udongo, wewe ndiye mfinyanzi; sisi sote tu kazi ya mkono wako.
Ni mimi nitangazaye mwisho tangu mwanzo, naam, tangu zamani za kale, mambo ambayo hayajatendeka. Ninasema: Kusudi langu ndilo litakalosimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.
Katika Kristo sisi nasi tumepata urithi, tukisha kuchaguliwa sawasawa na kusudi la Mungu, yeye ambaye hufanya mambo yote kulingana na kusudi la mapenzi yake,
Hatua za mtu huongozwa na Bwana. Anawezaje basi mtu yeyote kuelewa njia yake mwenyewe?
Siku za maisha yangu ziko mikononi mwako, uniokoe mikononi mwa adui zangu na wale wanifuatiao.