Mistari ya Biblia Kuhusu Bwana Huongoza Hatua Zetu
Mistari 8 ya Biblia kuhusu Bwana Huongoza Hatua Zetu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
BWANA huziongoza hatua za kila mtu, basi mtu awezaje kuelewa anakokwenda?
Watu hupanga njia zao mioyoni mwao, bali ni BWANA anayeziongoza hatua zao.
BWANA huzifanya hatua za mtu kuwa imara anapopendezwa na njia yake.
Mwamini BWANA kwa moyo wako mzima, wala usijiegemeze kwenye busara yako mwenyewe. Mkumbuke yeye katika kila unalofanya, naye atakutengenezea njia iliyonyooka mbele yako.
Nitakupa ufahamu na kukuonyesha njia unayopaswa kuifuata; nitakushauri na kukuangalia kwa jicho langu.
Mkabidhi BWANA kila unachofanya, na mipango yako itasimama imara.
kwamba huyu ndiye Mungu, Mungu wetu milele na daima; yeye atakuwa kiongozi wetu mpaka tufe.
Anawaelekeza wanyonge katika yaliyo ya haki, na wanyonge anawafundisha njia yake.