Mistari ya Biblia Kuhusu Mungu Anatawala

Mistari 8 ya Biblia kuhusu Mungu Anatawala ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 8 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 Zaburi 93:1 Mstari mkuu

BWANA ni Mfalme! Amevaa enzi kama joho; BWANA amejivika, akajifunga nguvu kama mshipi. Ulimwengu umesimama imara; hakuna kitakachoutikisa.

02 Zaburi 47:8

Mungu sasa anatawala kama Mfalme juu ya mataifa; juu ya kiti chake kitakatifu cha enzi Mungu ameketi.

03 Ufunuo 19:6

Nikasikia kitu kama sauti ya umati mkubwa mno, kama mvumo wa maji mengi na kama mshindo wa ngurumo zenye nguvu: “Haleluya! Kwa maana Bwana Mungu, Mwenyezi, ameanza kutawala.

04 Zaburi 96:10

Yaambieni mataifa, “BWANA ni Mfalme! Ulimwengu umesimama imara; hakuna kitakachoufanya uyumbe. Atawahukumu watu kwa haki.”

05 Zaburi 99:1

BWANA ni Mfalme; mataifa na yatetemeke! Ameketi juu ya makerubi kama juu ya kiti cha enzi; nchi na itikisike!

Mbingu na zijae furaha na nchi ishangilie; na itangazwe kati ya mataifa, “BWANA ni Mfalme!”

07 Zaburi 145:13

Ufalme wako ni ufalme wa zama zote, na utawala wako unadumu katika kila kizazi.

08 Kutoka 15:18

BWANA atatawala milele hata milele!”

Mada zinazohusiana