Mistari ya Biblia Kuhusu Mungu Hutenda Mambo Yote
Mistari 7 ya Biblia kuhusu Mungu Hutenda Mambo Yote ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Ndani yake sisi pia tumefanywa fungu la Mungu mwenyewe. Tuliamuliwa kwa ajili ya jambo hili tangu awali kwa kusudi la Mungu, anayetenda kila kitu kama mapenzi yake yanavyoamua,
Tunajua kwamba, kwa watu wanaompenda Mungu, mambo yote yanashirikiana na kuelekea kwenye mema. Hao ndio wale walioitwa kulingana na kusudi lake.
Kwa maana ndani yake vitu vyote viliumbwa, vya mbinguni na vya duniani, vinavyoonekana na visivyoonekana, viwe viti vya enzi au tawala, watawala au mamlaka. Vyote vimeumbwa kupitia yeye na kwa ajili yake. Yeye yupo kabla ya vitu vyote, na vitu vyote vinashikamana pamoja ndani yake.
Lolote ambalo BWANA anachagua kufanya, hulifanya, mbinguni, duniani, baharini na katika vilindi vyote vya bahari.
BWANA amefanya kila kitu kwa ajili ya mwisho wake, hata mwovu kwa ajili ya siku ya maafa.
Kwa maana vitu vyote vimetoka kwake, vipo kupitia yeye, na ni kwa ajili yake. Utukufu uwe kwake milele! Amina.
Kusudi la BWANA husimama imara milele, na yale aliyoyapanga moyoni mwake hudumu katika kila kizazi.