Mistari ya Biblia Kuhusu Bwana Mponyaji Wetu
Mistari 10 ya Biblia kuhusu Bwana Mponyaji Wetu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Alisema, “Ukisikiliza kwa makini sauti ya BWANA Mungu wako na kufanya yale anayoyaona kuwa sawa, ukizitii amri zake na kushika kanuni zake zote, nitakuepusha na kila mojawapo ya magonjwa niliyowaletea Wamisri. Kwa maana mimi ni BWANA ninayekuponya.”
Nafsi yangu, mbariki BWANA, wala usisahau kamwe yote aliyokutendea, ndiye anayekusamehe kila kosa lako, anayekuponya kila ugonjwa ulio nao,
Huwaponya wale ambao mioyo yao imepondeka na kuyafunga majeraha yao.
BWANA, Mungu wangu, nilikulilia unisaidie, nawe ukanipa afya.
Njooni kwangu, nyote mliochoshwa na kazi ngumu na kuelemewa na mizigo mizito, nami nitawapa pumziko.
Yeye mwenyewe alizibeba dhambi zetu katika mwili wake mwenyewe hadi msalabani, ili tuachane na dhambi na tuishi kwa ajili ya haki. Kwa majeraha aliyoyapata ninyi mmeponywa.
BWANA atawategemeza kitandani mwao wakiwa wagonjwa; wanapougua, unakigeuza kitanda chao chote cha ugonjwa kuwa afya.
“Roho wa Bwana anakaa juu yangu, kwa kuwa amenipaka mafuta ili niwapelekee maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kwamba wako huru, na vipofu kwamba wataona tena, kuwaweka huru wanaokandamizwa,
Alituma neno lake akawaponya; akawavuta kutoka katika shimo la mauti.
Je, kuna yeyote miongoni mwenu aliye mgonjwa? Awaite wazee wa kanisa, nao wamwombee na kumpaka mafuta katika jina la Bwana. Maombi yaliyofanywa kwa imani yatamwokoa mgonjwa, na Bwana atamwinua. Na kama ametenda dhambi, atasamehewa.