Mistari ya Biblia Kuhusu Kusafishwa kwa Moto

Mistari 14 ya Biblia kuhusu Kusafishwa kwa Moto ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 1 Petro 1:7

Haya yamewajia ili kwamba imani yenu, iliyo ya thamani kuliko dhahabu ipoteayo, ingawa hujaribiwa kwa moto, ionekane kuwa halisi na imalizie katika sifa, utukufu na heshima wakati Yesu Kristo atadhihirishwa.

02 Zekaria 13:9

Hii theluthi moja nitaileta katika moto; nitawasafisha kama fedha isafishwavyo na kuwajaribu kama dhahabu. Wataliitia Jina langu nami nitawajibu; nitasema, ‘Hawa ni watu wangu,’ nao watasema, ‘ Bwana ni Mungu wetu.’ ”

03 Malaki 3:3

Ataketi kama mfuaji na asafishaye fedha. Atawatakasa Walawi, naye atawasafisha kama dhahabu na fedha. Kisha Bwana atakuwa na watu watakaoleta sadaka katika haki,

04 Ayubu 23:10

Lakini anaijua njia niiendeayo; akiisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.

05 Isaya 48:10

Tazama, nimekusafisha, ingawa si kama fedha, nimekujaribu katika tanuru ya mateso.

06 Mithali 17:3

Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru ni kwa ajili ya dhahabu, bali Bwana huujaribu moyo.

07 Zaburi 66:10

Ee Mungu, wewe ulitujaribu, ukatusafisha kama fedha.

08 Isaya 1:25

Nitauelekeza mkono wangu dhidi yenu, nitawasafisha takataka zenu zote na kuwaondolea unajisi wenu wote.

09 Danieli 12:10

Wengi watatakaswa, na kuondolewa mawaa na kufanywa safi, lakini waovu wataendelea kuwa waovu. Hakuna mmoja wa waovu atakayefahamu, lakini wale wenye hekima watafahamu.

10 Yakobo 1:12

Heri mtu anayevumilia wakati wa majaribu, kwa sababu akiisha kushinda hilo jaribio atapewa taji la uzima Mungu alilowaahidia wale wampendao.

11 1 Wakorintho 3:13

kazi yake itaonekana ilivyo, kwa kuwa Siku ile itaidhihirisha. Itadhihirishwa kwa moto, nao moto utapima ubora wa kazi ya kila mtu.

12 Ayubu 42:5

Masikio yangu yalikuwa yamesikia habari zako, lakini sasa macho yangu yamekuona.

13 Warumi 5:3-5

Si hivyo tu, bali twafurahi pia katika mateso, kwa sababu tunajua kuwa mateso huleta saburi, nayo saburi huleta uthabiti wa moyo, na uthabiti wa moyo huleta tumaini, wala tumaini halitukatishi tamaa, kwa sababu Mungu amekwisha kumimina pendo lake mioyoni mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ametupatia.

14 2 Wakorintho 4:17

Kwa maana dhiki yetu nyepesi iliyo ya kitambo inatutayarisha kwa ajili ya utukufu wa milele unaozidi kuwa mwingi kupita kiasi,

Mada zinazohusiana