Mistari ya Biblia Kuhusu Mwili Mmoja, Viungo Vingi

Mistari 11 ya Biblia kuhusu Mwili Mmoja, Viungo Vingi ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 1 Wakorintho 12:12

Kama vile mwili ulivyo mmoja nao una viungo vingi, navyo viungo vyote vya mwili ingawa ni vingi, ni mwili mmoja, vivyo hivyo na Kristo.

02 1 Wakorintho 12:13

Kwa maana katika Roho mmoja wote tulibatizwa katika mwili mmoja, kama ni Wayahudi au Wayunani, kama ni watumwa au watu huru, nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.

03 1 Wakorintho 12:27

Sasa ninyi ni mwili wa Kristo na kila mmoja wenu ni sehemu ya huo mwili.

04 Warumi 12:4-5

Kama vile katika mwili mmoja tulivyo na viungo vingi, navyo viungo vyote havina kazi moja, vivyo hivyo na sisi tulio wengi, tu mwili mmoja katika Kristo, nasi kila mmoja ni kiungo cha mwenzake.

05 Waefeso 4:16

Kutoka kwake, mwili wote ukiwa umeungamanishwa na kushikamanishwa pamoja kwa msaada wa kila kiungo, hukua na kujijenga wenyewe katika upendo, wakati kila kiungo kinafanya kazi yake.

06 1 Wakorintho 12:14

Basi mwili si kiungo kimoja, bali ni viungo vingi.

07 1 Wakorintho 12:18

Lakini kama ilivyo, Mungu ameweka viungo katika mwili, kila kimoja kama alivyopenda.

08 1 Wakorintho 12:25

ili pasiwe na mafarakano katika mwili, bali viungo vyote vihudumiane kwa usawa kila kimoja na mwenzake.

09 Warumi 12:5

vivyo hivyo na sisi tulio wengi, tu mwili mmoja katika Kristo, nasi kila mmoja ni kiungo cha mwenzake.

10 Wakolosai 3:15

Amani ya Kristo na itawale mioyoni mwenu, kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena kuweni watu wa shukrani.

11 Waefeso 4:25

Kwa hiyo kila mmoja wenu avue uongo na kuambiana kweli mtu na jirani yake, kwa maana sisi sote tu viungo vya mwili mmoja.

Mada zinazohusiana