Mistari ya Biblia Kuhusu Watenda Kazi kwa Mavuno

Mistari 9 ya Biblia kuhusu Watenda Kazi kwa Mavuno ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Luka 10:2

Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini watendakazi ni wachache. Kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno, ili apeleke watendakazi katika shamba lake la mavuno.

02 Mathayo 9:37-38

Ndipo akawaambia wanafunzi wake, “Mavuno ni mengi lakini watendakazi ni wachache. Kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno, ili apeleke watendakazi katika shamba lake la mavuno.”

03 1 Wakorintho 3:9

Kwa kuwa sisi tu watendakazi pamoja na Mungu. Ninyi ni shamba la Mungu, jengo la Mungu.

04 Yohana 4:35

Je, ninyi hamsemi, ‘Bado miezi minne tuvune?’ Inueni macho yenu myaangalie mashamba jinsi mazao yalivyo tayari kuvunwa!

05 2 Wakorintho 6:1

Kama watendakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msipokee neema ya Mungu bure.

06 Mathayo 9:38

Kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno, ili apeleke watendakazi katika shamba lake la mavuno.”

07 1 Wakorintho 3:6-7

Mimi nilipanda mbegu, Apolo akatia maji, lakini Mungu ndiye aliikuza. Hivyo mwenye kupanda na mwenye kutia maji si kitu, bali Mungu peke yake ambaye huifanya ikue.

08 Wakolosai 4:11

Yesu, yeye aitwaye Yusto, pia anawasalimu. Hawa peke yao ndio Wayahudi miongoni mwa watendakazi wenzangu kwa ajili ya Ufalme wa Mungu, nao wamekuwa faraja kwangu.

09 Wafilipi 2:25

Lakini nadhani ni muhimu kumtuma tena kwenu Epafrodito, ndugu yangu na mtendakazi pamoja nami, aliye askari mwenzangu, ambaye pia ni mjumbe wenu mliyemtuma ili ashughulike na mahitaji yangu.

Mada zinazohusiana