Mistari ya Biblia Kuhusu Watendaji wa Neno

Mistari 11 ya Biblia kuhusu Watendaji wa Neno ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Yakobo 1:22

Basi kuweni watendaji wa Neno wala msiwe wasikiaji tu, huku mkijidanganya nafsi zenu.

02 Mathayo 7:24

“Kwa hiyo kila mtu ayasikiaye haya maneno yangu na kuyatenda, ni kama mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba.

03 Luka 11:28

Yesu akajibu, “Wamebarikiwa zaidi wale wanaolisikia neno la Mungu na kulitii.”

04 Yohana 13:17

Sasa kwa kuwa mmejua mambo haya, heri yenu ninyi kama mkiyatenda.

05 Warumi 2:13

Kwa maana si wale wanaoisikia sheria ambao ni wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale wanaoitii sheria ndio watakaohesabiwa haki.

06 Yakobo 1:25

Lakini yeye anayeangalia kwa bidii katika sheria kamilifu, ile iletayo uhuru, naye akaendelea kufanya hivyo bila kusahau alichosikia, bali akalitenda, atabarikiwa katika kile anachofanya.

07 Mathayo 7:21

“Si kila mtu aniambiaye, ‘Bwana, Bwana,’ atakayeingia katika Ufalme wa Mbinguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

08 Ezekieli 33:31

Watu wangu wanakujia, kama wafanyavyo, nao wanaketi mbele yako kama watu wangu na kusikiliza maneno yako, lakini hawayatendi. Kwa maana udanganyifu u katika midomo yao, lakini mioyo yao ina tamaa ya faida isiyo halali.

09 Yohana 14:15

“Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu.

10 1 Yohana 3:18

Watoto wapendwa, tusipende kwa maneno au kwa ulimi bali kwa tendo na kweli.

11 Tito 1:16

Wanadai kumjua Mungu, lakini kwa matendo yao wanamkana. Hao watu ni chukizo, wasiotii, wasiofaa kwa jambo lolote jema.

Mada zinazohusiana