Mistari ya Biblia Kuhusu Mkanganyiko

Mistari 9 ya Biblia kuhusu Mkanganyiko ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 1 Wakorintho 14:33

Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko bali ni Mungu wa amani. Kama ilivyo katika makusanyiko yote ya watakatifu,

02 Yakobo 3:16

Kwa maana panapokuwa na wivu na ubinafsi, ndipo penye machafuko na uovu wa kila namna.

03 Yakobo 1:5

Kama mtu yeyote miongoni mwenu amepungukiwa na hekima na amwombe Mungu, yeye awapaye watu wote kwa ukarimu wala hana kinyongo, naye atapewa.

04 Isaya 26:3

Utamlinda katika amani kamilifu yeye ambaye moyo wake ni thabiti kwa sababu anakutumaini wewe.

05 Mithali 3:5-6

Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako.

06 Yohana 14:27

Amani nawaachia, amani yangu nawapa, amani hii niwapayo si kama ile ulimwengu utoayo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.

07 Zaburi 32:8

Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; nitakushauri na kukuangalia.

08 Yeremia 29:11

Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu,” asema Bwana, “ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo.

09 Wakolosai 2:2-3

Kusudi langu ni watiwe moyo na kuunganishwa katika upendo, ili wapate ule utajiri wa ufahamu mkamilifu, ili waijue siri ya Mungu, yaani, Kristo mwenyewe, ambaye ndani yake kumefichwa hazina zote za hekima na maarifa.

Mada zinazohusiana