Mistari ya Biblia Kuhusu Tafakarini Mambo Haya

Mistari 5 ya Biblia kuhusu Tafakarini Mambo Haya ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Wafilipi 4:8

Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo na sifa njema, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote ya kupendeza, yoyote yenye staha, ukiwepo uzuri wowote, pakiwepo chochote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo.

02 Wakolosai 3:2

Yafikirini mambo yaliyo juu, wala si ya duniani.

03 Warumi 12:2

Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kuonja na kuhakikisha ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na ukamilifu.

04 2 Wakorintho 10:5

tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu, na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo,

05 Zaburi 19:14

Maneno ya kinywa changu na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu na Mkombozi wangu.

Mada zinazohusiana