Mistari ya Biblia Kuhusu Akili Thabiti
Mistari 10 ya Biblia kuhusu Akili Thabiti ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Habari mbaya haziwatishi; mioyo yao iko imara kwa sababu wanamtumaini BWANA.
Basi, ndugu zangu wapendwa, simameni imara bila kutikisika, mkizidi kufanya kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa mnajua kwamba katika Bwana kazi yenu ngumu haipotei bure.
Yeye ni mwenye nia mbili, hana msimamo katika yote anayofanya.
Tumkazie macho Yesu, kiongozi aliyetutangulia katika imani na anayeikamilisha. Kwa ajili ya furaha iliyokuwa mbele yake, alivumilia msalaba na kuihesabu aibu yake kuwa si kitu, kisha ameketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.
ikiwa tu mnadumu katika imani, mkiwa imara juu ya msingi wenu na thabiti, bila kuyumbishwa mbali na tumaini mlilopewa katika Injili mliyoisikia. Injili hii imehubiriwa kwa kila kiumbe chini ya mbingu, nami Paulo nimekuwa mtumishi wake.
Baada ya kuteseka kwa muda mfupi, Mungu wa neema zote, aliyewaita kwenye utukufu wake wa milele katika Kristo, yeye mwenyewe atawarejesha, atawafanya imara na wenye nguvu, na kuwasimika juu ya msingi thabiti.
Moyo wangu ni imara, Ee Mungu, moyo wangu ni imara; nitaimba na kupiga nyimbo za sifa.
Kwa hiyo, ndugu, endeleeni kusimama imara, na myashike kwa nguvu mapokeo tuliyowafundisha, iwe tuliyasema ana kwa ana au tuliyaandika katika barua yetu.
Nina hakika na jambo hili: aliyeanza kazi njema ndani yenu ataendelea nayo mpaka aikamilishe siku ya Kristo Yesu.
Tuushikilie ukiri wa tumaini letu bila kulegea hata kidogo, kwa kuwa yule aliyetoa ahadi hiyo ni mwaminifu.