Mistari ya Biblia Kuhusu Ungama na Uamini
Mistari 6 ya Biblia kuhusu Ungama na Uamini ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Ongeza mistari yote 6 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
Ukitangaza kwa kinywa chako kwamba Yesu ni Bwana, na ukaamini kwa moyo wako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, basi utaokolewa. Kwa maana watu huamini kwa moyo, na hilo huwaletea haki; hukiri kwa kinywa, na hilo huwaletea wokovu.
02 Warumi 10:13
Kwa maana “wote watakaoliitia jina la Bwana wataokolewa.”
Basi kila mtu atakayesema waziwazi mbele ya watu kwamba yeye ni wangu, nami nitamtambua mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.
Mtu yeyote anapokiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu anakaa ndani yake, naye anakaa ndani ya Mungu.
Wakamjibu, “Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokolewa, wewe pamoja na watu wa nyumbani mwako.”
06 Warumi 10:11
Kwa maana Maandiko yanasema, “Yeyote anayemwamini hataaibika.”