Mistari ya Biblia Kuhusu Kuenenda kwa Imani
Mistari 7 ya Biblia kuhusu Kuenenda kwa Imani ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
kwa maana tunaishi kwa imani, si kwa kuona.
Na hakuna anayeweza kumpendeza Mungu bila imani, kwa sababu kila anayemkaribia Mungu hana budi kuamini kwamba yeye yuko, na pia kwamba huwalipa wale wanaomtafuta kwa bidii.
Ndani ya Injili haki ya Mungu inafunuliwa, kutoka imani kwa ajili ya imani. Kama ilivyoandikwa, “Mtu aliye mwenye haki ataishi kwa imani.”
Si mimi tena ninayeishi; Kristo ndiye anayeishi ndani yangu. Maisha yoyote ninayoishi bado katika mwili, ni maisha ya imani katika Mwana wa Mungu, aliyenipenda na kujitoa mwenyewe kwa ajili yangu.
Mlimpokea Kristo Yesu kuwa Bwana. Kwa hiyo maisha yenu yote yawe ndani yake,
Kwa imani Ibrahimu alitii wito wa Mungu wa kuondoka kwenda nchi ambayo baadaye angepewa kuwa yake mwenyewe, naye akaanza safari bila kujua alikokuwa akielekea.
Hakuwa na shaka juu ya ahadi ya Mungu, wala hakusitasita kwa kutoamini. Badala yake imani yake ilipata nguvu, akampa Mungu utukufu, akiwa na hakika kamili kwamba Mungu ana uwezo wa kutimiza kile alichoahidi.