Mistari ya Biblia Kuhusu Ngao ya Imani
Mistari 8 ya Biblia kuhusu Ngao ya Imani ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Katika kila hali shikeni imani kama ngao yenu; kwayo mtaweza kuzima mishale yote ya moto ya yule mwovu.
Jivikeni silaha kamili za Mungu, ili mweze kusimama imara mbele ya mipango ya hila ya Ibilisi.
Simameni imara dhidi yake, mkiishikilia imani yenu. Mnajua kwamba ndugu zenu kote ulimwenguni wanavumilia mateso hayo hayo.
BWANA ni nguvu yangu, ngao inayonilinda; moyo wangu ulimtumaini, nami nikapata msaada. Sasa moyo wangu umejaa furaha, nami nitamshukuru kwa wimbo.
kwa sababu kila kilichozaliwa na Mungu kinaushinda ulimwengu. Na imani yetu ndiyo ushindi ulioushinda ulimwengu.
Tunajua kwamba kila aliyezaliwa na Mungu haendelei kutenda dhambi; badala yake, Mwana, aliyezaliwa na Mungu, humlinda salama, na yule mwovu hamshiki.
Kila neno asemalo Mungu limethibitika kuwa kweli; yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake.
Lakini Bwana ni wa kuaminika: atawafanya imara na kuwalinda dhidi ya yule mwovu.