Mistari ya Biblia Kuhusu Imani bila Matendo Imekufa
Mistari 6 ya Biblia kuhusu Imani bila Matendo Imekufa ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Ndivyo ilivyo kwa imani: ikiwa haina matendo, imekufa ndani yake yenyewe.
Kama mwili usio na roho ndani yake ulivyo mfu, ndivyo na imani isiyo na matendo ilivyo mfu.
Lakini mtu atasema, “Wewe una imani, nami nina matendo.” Nionyeshe imani yako isiyo na matendo yoyote, nami nitakudhihirishia imani yangu kupitia matendo yangu.
Kwa maana katika Kristo Yesu, tohara au kutotahiriwa havina thamani yoyote. Kinachohesabika ni imani inayofanya kazi kwa njia ya upendo.
Si kila mtu anayeniita ‘Bwana, Bwana’ ataingia katika ufalme wa mbinguni, ila wale tu wanaofanya yale ambayo Baba yangu wa mbinguni anataka.
Basi mnaona kwamba ni kwa matendo mtu anahesabiwa haki, wala si kwa imani pekee.